Jumatano 7 Mei 2025 - 09:32
Mufti wa Zanzibar aongoza kikao cha kamati ya amani mbele ya Raisi Mwinyi

Hawza/ Mufti wa Zanzibar ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya amani Zanzibar, ameongoza kikao cha kamati hiyo huku kikao hicho kikihudhuriwa na Raisi wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ally Mwinyi.

 Shirika la Habari la Hawza - Mwenyekiti wa kamati ya amani ambae pia ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaab, ameongoza kikao cha amani kilicho andaliwa chini ya Raisi wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ally Mwinyi, kikiwa na anuani ya kujadili mustakabali wa amani kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu.

Katika kikao hicho mwenyekiti huyo wa amani Zanzibar amesema: Mkakati wa kamati hiyo ni kuhakikisha mazingira ya uchaguzi yanakuwa ya amani wakati wa uchaguzi, na baada ya uchaguzi, na wananchi waingie katika uchaguzi kwa uwazi, upendo na furaha. 

Nae Rais Mwinyi ameihakikishia kamati hiyo kuwa, Serikali inafanya kila juhudi kuhakikisha mifumo yote ya uchaguzi inafanya kazi kwa  uhuru ,Amani na uwazi wakati wa kampeni, upigaji kura na matokeo ya uchaguzi, kwa dhamira ya kudumisha amani iliopo kwa ajili ya maslahi ya nchi.

Dkt, Mwinyi ameishauri kamati hiyo kuwakutanisha wanasiasa na kufanya Mjadala wa pamoja ili Kuzungumzia umuhimu wa amani ya nchi pamoja na kudhibiti viashiria  vya uvunjifu wa amani kabla na baada ya uchaguzi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha